Local Bulletins

Wakaazi wa Marsabit wataka kutekelezwa kwa miradi ambayo imejumuishwa kwenye programu ya maendeleo katika kipindi cha 2023-2027

Na Caroline Waforo

Wakaazi katika kaunti ya Marsabit wametaka kutekelezwa kwa miradi ya maendeleo ambayo imejumuishwa katika ruwaza ya serikali kuu ya mwaka 2023/27.

Wakitoa maoni yao katika uzinduzi wa nne wa mpango wastani ambao unajumuisha kipindi cha mwaka 2023-2027, kikao cha kuhusisha umma na ufafanuzi wa programu ya maendeleo katika kaunti ya Marsabit, hafla iliyoandaliwa katika ukumbi wa kanisa katoliki, wakaazi hao wakiongozwa na Nuria Golo ambaye  ni mwasisi wa shirika lisilo la kiserikali la MWADO wamesema kuwa kwa wakati mwingi ahadi zinatolewa lakini hazitekelezwi.

Nuria pia ameitaka serikali kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa miradi ya mabwawa na visima inatunzwa ili kuzuia uharibifu.

Wakaazi hao aidha wamekosoa mfumo wa ugavi wa raslimali wa one man one vote one shilling wakilalama kuwa utabagua jimbo hili na maeneo mengine kame.

Wario Yattani almaarufu Ole Woiye na ambaye alikuwa mwaniaji wa kiti cha ugavana kaunti ya Marsabit katika uchaguzi wa 2022 alizungumza kwa niaba ya wakaazi.

Pia amekashifu Viongozi hapa jimboni Marsabit Kwa kususia hafla ya Leo.

Subscribe to eNewsletter