Local Bulletins

WAKAAZI WA MARSABIT WATAHADHARISHWA DHIDI YA KUTUMA MAOMBI YA ID ZAIDI YA MARA MOJA.

Na Caroline Waforo

Wakaazi kaunti ya Marsabit wametahadharishwa dhidi ya kutuma maombi ya kupata vitambulisho zaidi ya moja.

Akizungumza na Shajara afisini mwake afisa wa usajili jimboni Marsabit Michael Oduor amesema kuwa hili litahitilafiana na shughuli za kuchapisha vitambulisho.

Hii ni kutokana na malalamishi ya kucheleweshwa kwa vitambulisho kutoka kwa baadhi ya wakaazi ambapo anasema kuwa mara kwa mara wakaazi wanaamua kutuma maombi tena.

Itakumbukwa kuwa vinavyochapishwa ni vitambulisho vya kidigitali maisha card.

Afisi ya usajili Marsabit imetuma maombi ya vitambulisho hivyo takriban 18,973.

Aidha Vitambulisho vya kidigatli 12,590 vimechapishwa na kutumwa jimboni huku 12,388 tayari vikiwa vimechukuliwa.

Subscribe to eNewsletter