Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Na Talaso Huka
Wakaazi wa Marsabit wanaoishi karibu na misitu wameshauri kukoma kulisha mifugo yao ndani ya msitu hadi wakati wa kiangazi.
Akizungumza na Radio Jangwani Naibu msisamizi wa idara ya msitu Kadiro Oche amewataka wafugaji kuzidi kutumia nyasi zilizopo malishoni mwanzo kabla ya kuvamia misitu kwa ajili ya malisho.
Vile vile Kadiro amewataka wanamarsabit kuhifadhi nyasi iliyoko sehemu ya malisho kwa sasa ili kuwasadia wakati wa kiangazi.
Aidha Kadiro amesema kuwa kuchomeka misitu au sehemu za malisho mara nyingi pia huathiri ukuaji wa nyasi ya mifugo akitaja hasara hiyo kuchangiwa pakubwa na watu wanaovuna asali na kuwacha moto bila kuzima. Kauli yake hiyo inajiri baada ya mioto kushuhudiwa katika sehemu za kulisha mifugo Hulahula na Kargi siku za maajuzi.
Hata hivyo Kadiro amewahimiza wanamarsabit kuwa waangalifu na kulinda misitu kwa kuwa inawasaidia kutimiza kimahitaji yao wakati wa kiangazi.