Idadi chache ya wanafunzi waripoti shuleni wiki ya kwanza ya muhula huu…
January 10, 2025
NA CAROLINE WAFORO
Huku ulimwengu ukiadhimisha Siku ya Mazingira Duniani, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mazingira Taifa (NEMA) Naftaly Osoro amebainisha umuhimu wa wakaazi wa Kaunti ya Marsabit kushiriki kikamilifu katika shughuli za utunzaji wa mazingira.
Kwa mujibu wa Osoro, ushiriki wa wakaazi katika utunzaji wa mazingira utasaidia sana katika kukomesha kuenea kwa majangwa na kukabiliana na changamoto za kiangazi kinachoongezeka katika eneo hilo.
Aidha, Osoro amesema kuwa NEMA kwa ushirikiano na Wizara ya Mazingira wanafanya jitihada za kutekeleza sheria mpya kuhusu mapato yanayotokana na udhibiti wa mabadiliko ya tabianchi, kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Mabadiliko ya Tabianchi ya mwaka 2023.
Hivyo, Osoro anawaasa wakaazi wa Marsabit kushiriki kikamilifu katika shughuli za kulinda na kurejesha mazingira ili kukabiliana na changamoto kama vile majangwa na kiangazi kinachoongezeka katika kaunti hiyo.