Idadi chache ya wanafunzi waripoti shuleni wiki ya kwanza ya muhula huu…
January 10, 2025
Na Isaac Waihenya & Naima Abdulahi
Wakaazi wa eneo la Laisamis wameitaka idara ya kilimo sawa na serekali ya kaunti kuharakisha kuwanyuzia dawa nzige wa Jangwani ambao wameonekana katika eneo hilo kwa kipindi cha wiki moja sasa.
Wakizungumza na Radio Jangwani kwa njia ya simu wakaazi hao Wakiongozwa na Ali Kochale,Ekai Lambire, na Francis Lekhoyan wamewataja nzige hao kama tishio kubwa kwa usalama wa chakula cha binadamu na hata cha mifugo.
Aidha wakaazi hao wamelezea wasiwasi wao kwamba uwepo wa wadudu hao unaweza kuwaresha katika hatari ya ukosefu wa lishe kama ilivyo shuhudiwa miaka ya nyuma huku wakiyataka mashirika yasiyo yakiserekali kushirikiana ili pia kuwaangamiza wadudu hao.