Local Bulletins

WAKAAZI WA HURI HILLS, MARSABIT WAPANDA ZAIDI YA MICHE 2000 KAMA NJIA MOJA YA KUKABILI TABIA NCHI.

Wakazi wa eneo la Huri Hills kaunti ya Marsabit wameweza kupanda Zaidi ya miti 2000 hii leo.

Akizungumza na idhaa hii, katekista wa Huri Hills Daniel Sifuna amesema kuwa kupitia msaada kutoka kwa shirika la Welt na KWS waliweza kupanda miche ambayo itasaidia katika kupunguza makali ya ukame na mafuriko katika eneo hilo.

Sifuna amesema kuwa ni wajibu wa kila mmoja kupanda miti ili kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.

Sifuna amewachangamoto wakazi wa Huri Hills kuchukua fursa hii ya kupata miche bure kupanda miti katika boma zao.

Vile vile Katekista Sifuna ametoa rai kwa mashirika yasiyo ya kiserekali ambayo yanashughulikia masuala ya mazingira kuweza kuwasaidia wakazi wa Huri hills kwa kuwaletea miche ya kutosha na pia kutoa mafunzo juu  ya Mazingira bora.

Subscribe to eNewsletter