Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
Wakaazi wa eneo la Funan Qumbi, lokesheni ya Rawana, kaunti ndogo ya Sololo eneo bunge ya Moyale kaunti ya Marsabit wamelalamikia hatua ya serekali ya kaunti ya Marsabit kutowafikishia tanki 14 za maji ambazo zilikuwa zimeratibiwa kupelekwa katika eneo hilo.
Wakiwakilishwa na Galm Sora ambaye ni mwenyekiti wa vijana katika eneo hilo, wamesema kuwa tanki hizo ambazo zilikuwa zimeratibiwa kuletewa wakazi wa Funan Qumbi tangu machi mwaka huu hazikufikishwa na badala yake ziliweza kuachwa kilomita 13 kutoka kwa Kijiji chao.
Akizungumza na idhaa hii, Galm amesema kuwa baadhi ya hizo tenki zimeweza kuharibika kwa sababu ya kukosa kutumika na hata kukosa ulinzi unaofaa.
Galm ameelezea kuwa licha ya juhudi zao za kufuatilia na kupata haki ya kuletewa tenki hizo , bado hawajafanikiwa jambo ambalo ametaja kwamba imelemaza upatikanaji na uhifadhi wa maji katika eneo hilo.
Anasema kuwa changamoto nyingine inayokumba Kijiji hicho ni kisima ambacho kimeharibika katika eneo hilo hivyo kusababisha wanakijiji kukosa maji.
Kadhalika Galm amesema kuwa wakazi wa Funan Qumbi bado wanaathirika na ukosefu wa chakula kwa sababu ya ukame ambao ulikuwa umekumba eneo hilo hivyo kurai wahisani pamoja na serekali kuweza kuwaletea wakazi hawa chakula cha msaada.