Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Idadi ya wagonjwa wa kifua kikuu TB na ambao pia wanaishi na virusi vya ukimwi iko chini humu jimboni Marsabit.
Haya ni huku visa vya ugonjwa wa kifua kikuu vikiongezeka katika kaunti hii ya Marsabit.
Haya ni kulingana na afisa anayesimamia magonjwa ya TB Sori Gone ambaye amezungumza na shajara ya radio jangwani kwa njia ya simu, akiweka wazi kuwa kufikia mwezi Novemba mwaka huu wa 2024 visa 645 vya ugonjwa wa kifua kikuu vilinakiliwa. Kati ya visa hivyo asilimia 8 inajumuisha wagonjwa wa TB wanaoishi na virus vya ukimwi.
Sori ameambatanisha ongezeka la ugonjwa wa kifua kikuu na sababu mbalimbali ikiwemo hali ya umaskini miongoni mwa jamii za Marsabit.
Haya ni huku ikibainika kuwa wanaume ndio huathirika pakubwa na ugonjwa wa kifua kikuu jimboni.
Vile vile amewataka wakaazi kuhakikisha wanajiepusha na ugonjwa wakifua kikuu kwa kuhakikisha kuwa wanaishi katika mazingira bora huku pia akiwataka wagonjwa wa kifua kikuu kuwaepusha wenzao kwa kuchukua tahadhari kama anavyoeleza.
Sori kadhalika amewataka wakaazi jimboni Marsabit kutupilia mbali dhana ya uhusiano kati ya ugonjwa wa kifua kikuu na ule wa virusi vya ukimwi akisema kuwa inaleta unyanyapaa dhjidi ya wagonjwa wa lkifua kikuu jimboni.
Kulingana na afisa huyu wa afya ugonjwa wa kifua kikuu huambukizwa kutoka mtu moja hadi mwengine. Mgonjwa moja wa kifua kikuu anaweza kuambukiza watu 15 kwa mwaka iwapo hatapokea matibabu.
Vilevile Sori amewataka wadau wote wakijumuisha serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali kushirikiana na idara yake katika kupambana na maambuzki ya ugonjwa wa kifua kikuu.