Idadi chache ya wanafunzi waripoti shuleni wiki ya kwanza ya muhula huu…
January 10, 2025
NA CAROLINE WAFORO
Wakaazi kaunti ya Isiolo wamefanya maandamano ya Amani kupinga mswada wa kifedha wa mwaka wa 2024. Wakaazi hao an ambao idadi kubwa ni vijana wamesema mswada huu unalenga kuwakadamiza wakenya ambayo tayari wanakabiliwa na mzigo mzito wa kiuchumi.
Waandamanaji hao wamesema kuwa hawajaona manufaa ya ushuru ambao wakenya wamekuwa wakitozwa kuambatana na sharia ya fedha ya waka 2023.
Wakati uo huo wamewataka wabunge wa Isiolo akiwemo Mumina Bonaya, Joseph Samal na Mohammed Tupi kupiga kura ya kupinga mswada huo bungeni