Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Wakaazi jimboni Marsabit wametakiwa kuripoti visa vyovyote vya uhalifu msimu huu wa sherehe za krismasi na mwaka mpya.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee OCPD wa Marsabit ya kati Edward Ndirangu amewataka wananchi kutoa taarifa zozote muhimu akisema kuwa hilo litasaidia katika kukabiliana na utovu wa usalama na ambao hushuhudiwa msimu huu wa sherehe katika maeneo mengi nchini.
Itakumbukwa kuwa pia wamiliki na waendesha magari jimboni wametakiwa kuhakikisha kuwa wanafuata sheria za trafiki ili kuepukana na ajali za barabarani na ambazo pia huongezeka msimu huu.