Marsabit yatajwa kuwa miongoni mwa kaunti zinazokuwa kwa kasi kimaendeleo.
January 15, 2025
Jamii za kaunti ya Marsabit zimehamasishwa kuhusu jinsi ya kujipanga na kupunguza makali ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Mafunzo hayo kwa wafugaji yamefadhiliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la CRDD linaloshughulikia umuhimu wa rasilimali na changamoto wanazopitia jamii ya wafugaji.
Akizungumza katika hafla hiyo, Rose Orguba ambaye ni mwanaharakati wa haki za binadamu amesema kuwa shirika hilo linasaidia jamii kujua dalili za mapema za mabadiliko ya hali ya hewa ili kukabiliana na madhara yake.
Aidha, Galma Dabaso ambaye ni naibu mwenyekiti wa shirika la DORIA la marsabit, pia akizungumza amesema kuwa takriban watu 40 kutoka maeneobunge yote wamekongamana kwa minajili ya kupata mafunzo hayo ili waweze kuwaelimisha wafugaji wanaoishi mashinani.
Vile vile, badhi ya wafugaji wameelezea mafunzo walioweza kupata katika hafla hiyo ambayo ni njia mbalimbali za kukabiliana na ukame.