Local Bulletins

WAFUGAJI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT WAHIMIZWA KUKUMBATIA KILIMO BIASHARA KAMA NJIA MOJA WAPO YA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI.

Na Grace Gumato,

Wafugaji katika kaunti ya Marsabit wamehimizwa kukumbatia kilimo Biashara kama njia moja wapo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza na idhaa hii ofisi mwake afisa wa kilimo katika eneo bunge la Saku Dub Nura ametaja kuwa wafugaji wanafaa kuwa na mfumo mbadala ya kijikumu kimaisha kama njia ya kuepuka kuwapoteza mifugo wao.

Aidha afisa huyo amewahimiza wafugaji kukumbatia kilimo kama moja wapo ya njia ambayo itasaidia kujikimu kimaisha na viile kuepukana na baa la njaa.

Hata hivyo kwa swala la punda kupungua katika kaunti ya Marsabit Dub amesema kuwa wafugaji wengi hawajui faida za punda na pia hawawadhamini huku akiwarai kuwatunza kama wanavyotunza mifugo wengine.

Subscribe to eNewsletter