Levaquin: Comprehensive Guide on Usage, Benefits, and Safety
December 20, 2024
Na Isaac Waihenya & Abdilaziz Abdi,
Wafanyikazi wa nyanjani CHPs katika kaunti ya Marsabit watalipwa mishara yao ya mwezi Julai, Agosti na Septemba hivi karibuni.
Haya ni kwa mujibu wa mshirikishi wa huduma za jamii katika kaunti ya Marsabit Abdi Yusuf.
Akizungumza na wahudumu wa afya hao wa nyanjani katika hospitali ya rufaa ya Marsabit wakati wa zoezi la uzinduzi la bima mpya ya afya ya SHA, Yusuf ametaja kwamba serekali ya kaunti inajiza titi kuhakikisha kwamba wahudumu hao wa afya wanapata malipo yao ili kuwawezesha kuendeleza shughuli zao za kila siku.
Aidha Yusuf ameweka wazi kuwa wahudumu hao wa afya wa nyanjani wataendeleza kampeni ya kuwasajili watu katika bima ya SHIF mashinani ili kuhakikisha kwamba kila mwananchi amesajiliwa huku akariri kuwa zoezi hilo linalenga kaya elfu mia moja katika kaunti ya Marsabit.
Hata hivyo Yusuf ameweka wazi namna ya kujisajili kuwa mwanachama katika bima hiyo mpya ya SHA.
Mtu akihitajika kubonyeza *147# na kisha kufuata maagizo.