Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Wachezaji wa timu ya Moite kutokoka eneo la Moite, wadi ya Loiyangalani wamelalamikia kutelekezwa na waadaaji wa kombe la Rasso Cup ambalo liliandaliwa katika eneo Loiyangalani na kukamilika mnamo tarehe 7 mwezi huu wa Disemba.
Kwa mujibu wa George Etir ambaye ni mmoja wa viongozi wa kikosi hicho amesema kuwa wachezaji hao wameachwa hoi licha ya makubaliano na waadaji wa michuano hiyo kwamba wangeshughulikiwa na vyakula wakati wa michuano sawa na mbinu za usafiri za kufika kushiriki sawa na kurejea eneo la moite baada ya michuano hiyo kukamilika.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee, Etir amesema kuwa wachezaji hao ambao wengine wao ni wa chini ya umri wa miaka 18 wamekuwa wakihangaika bila chakula, maji na hata mahala pa kulala kwa muda wiki moja na nusu huku kukiwa hakuna matumaini ya kupata msaada kutoka kwa waandalizi wa michuano hiyo Damaris Kewap pamoja na mbunge wa Saku Dido Ali Rasso.
Aidha Etir amelalama kwamba hata licha ya kutumia fedha zao kusafiri hadi Loiyangaliani waandalizi wa michuano hiyo wakiongozwa na Damaris Kewap wamedida kurejesha fedha hizo.
Vilevile Etir amefichua kwamba walioshinda katika nafasi mbalimbali za michuano hiyo hawakopokea zawadi zao kamawalivyoahidiwa huku zawadi ikitolewa kwa nambari moja pekee.
Kuhusiana na swala na vilabu vya eneo la Loiyangalani kutotambuliwa na shirikisho la mpira wa miguu wa nchini FKF Etir ameiwata mahodha kuhakikisha kwamba wamejisajili na shirikisho hilo ili kusaidia vijana kupiga hatua kitalanta.