Local Bulletins

WABUNGE 195 DHIDI YA 106 WAPIGA KURA YA NDIO KWENYE MAREKEBISHO YA MSWADA TATA WA FEDHA

NA SAMUEL KOSGEI

Jumla ya wabunge 195 wamepiga kura ya ndio kuunga mkono mswada tata wa fedha ambao umepokea pingamizi kubwa kutoka kwa umma huku huku wabunge 106 na wakipiga kura ya kuupinga. Kura tatu zikiharibika.

Hatua hiyo ilijiri huku maelfu ya Wakenya wakiingia barabarani katika miji mbalimbali wakiandamana kupinga Mswada tata wa Fedha wa 2024. Kura hiyo sasa inaashiria kuwa mswada huo sasa hadi utasonga hadi hatua ya Tatu.

Siku ya Jumanne (leo), Mswada wa Sheria ya Fedha ulienda kwa Kamati ya Bunge zima, ambapo kila marekebisho yalipigiwa kura kifungu baada ya kifungu.

Iwapo wabunge hao watapitisha mswada huo katika hatua ya Kusomwa kwa Mara ya Tatu, utatumwa kwa Rais William Ruto ili aidhinishwe kuwa sheria.

Wakati huo huo, wabunge wataanza mapumziko ya wiki mbili Ijumaa, Juni 28, kufuatia kukamilika kwa shughuli zinazohusiana na bajeti katik

 

Subscribe to eNewsletter