Idadi chache ya wanafunzi waripoti shuleni wiki ya kwanza ya muhula huu…
January 10, 2025
Na Talaso Huka
Waakazi wa Marsabit wametoa hisia zao kutokana na makundi ya vijana maarufu kama ‘Gen Z’ kujihusisha kwenye maandamano ya kuupinga mswada wa fedha wa mwaka 2024/2025.
Baadhi ya wakaazi waliozungumza na idhaa hii wametoa maoni yao kuwa wanaunga mkono vijana kukua mstari wa mbele kuongoza maandamano kwa kuwa wanatetea haki yao kama vijana.
Aidha baadhi ya wakaazi hao pia wamesema kuwa hawaungi mkono mswada ya fedha wa mwaka 2024/25 kwa sababu inawakandamazia maslahi yao kama wananchi.
‘’Biashara italemaa kutokana na uwepo wa ushuru mkubwa nchini. Viwanda haviwezi kukua, hivyo kupotea ajira kwa vijana nchin’’ asema mmoja wa wakaazi wa mji wa Marsabit.
Hata hivyo wengine wanasema kuwa wanaunga mkono mswada huo wa fedha na wakisema kuwa wanakubaliana na mpango wa serikali kukusanya hela za kufanya maendeleo.