Idadi chache ya wanafunzi waripoti shuleni wiki ya kwanza ya muhula huu…
January 10, 2025
Na Grace Gumato
Idadi ya visa vya dhulma ya kinjisia katika kaunti ya Marsabit vinazidi kuongezeka maradufu kutoka na mabadiko ya Tabianchi.
Akizungumza na idhaa hii afisini mwake Abraham Dale ambaye ni afisa wa shirika la kutetea maslahi ya wanawake MWADO ni kuwa visa vya ukeketaji ya watoto wa kike ni asilimia 88 na ndoa za mapema zikiwa ni asilimia 29 idadi ambayo anasema kuwa iko juu zaidi.
Aidha Dale amesema kuwa idadi hii imeogezeka kwa sababu ya utamaduni mbovu ambayo inachangia wasichana wengi kukeketwa na pia tabia nchi ambayo imechangia pakubwa katika dhulma za kinjinsia miongoni mwa wafugaji.
Hata hivyo Dale amehimiza jamii za Marsabit kutokuwa kimya kuhusiana na swala la dhulma za kinjisia akisema wahadhiriwa wanafaa kuripoti visa hivyo kwa idara husika ili kupata usaidizi.
Wito huo unajiri huku dunia hii leo ikiadhimisha siku ya dhidi ya dhulma za kijinsia.