Local Bulletins

VIONGOZI WA VIJANA KATIKA LOKESHENI YA NAGAYO ENEOBUNGE LA SAKU, KAUNTI YA MARSABIT WATAKA VIONGOZI KUANGAZIA MASWALA UKOSEFU WA AJIRA.

Na Johnbosco Nateleng

 

Kiongozi wa vijana katika lokesheni ya Nagayo eneo bunge la Saku, kaunti ya Marsabit Hussein Liban Boru ametaka viongozi kuangazia maswala ya kuwainua vijana katika eneo hilo kwani vijana wengi hawana kazi.

Boru amesema kuwa kwa manufaa ya vizazi vijavyo ni sharti viongozi wajitolee na kuwahamazisha vijana ambao wamekuwa watumwa waadawa za kulevya na pia kutumika na viongozi kusababisha vurugu.

Ametaka viongozi wa kaunti kujitokeza na kuwapa msaada vijana ili kujiinua na kujiajiri ili wasije wakapotoka kwani vijana ndio nguzo ya jamii.

Boru hata hivyo ameeleza kuwa licha ya wao kuungana na kuja pamoja kama vijana bado viongozi wanawapuuza kwani hawapati usaidizi wowote toka kwa viongozi hawa.

Kwenye suala la michezo Boru amewataka viongozi kujikakamua katika kukarabati uwanja wa michezo ya Marsabit ili kuwafanya vijana kuboresha na kujitokeza kuonyesha talanta zao.

Wakti uo huo amewataka vijana kujitokeza na kushirikiana na kuwa katika mastari wa mbele wa kuwa wabunifu katika kuanzisha biashara yao ya kibinafsi kuliko kujitosa katika matumizi ya dawa za kulevya ambayo haisaidii.

Subscribe to eNewsletter