Local Bulletins

VIONGOZI WA KISIASA NA WA KIJAMII KUTOKA MAENEO YA DUKANA, TURBI, MAIKONA NA NORTH HORR WAMEPEWA HAMASA KUHUSIANA NA NAMNA NA FAIDA ZA KUSAJILI ARDHI YA JAMII.

Na Isaac Waihenya,

Viongozi wa kisiasa na wa kijamii kutoka maeneo ya Dukana, Turbi, Maikona na North Horr wamepewa hamasa kuhusiana na namna na faida za kusajili ardhi ya jamii katika kaunti ya Marsabit.

Kwenye mkao ulioandaliwa hii leo na mashirika yasiyoyakiserekali ya IREMO na PISP ambao umewalata pamoja, MaMCAs wa wadi za Dukana, Turbi/Bubisa, North Horr pamoja na baraza la wazee la jamii ya Gabra, viomgozi hao kwa ujumla wamekubaliana hoja ya ardhi za jamii hapa jimboni kusajili ili kuwapa haki ya umiliki wannchi wa jimbo hili.

Akizungumza wakati wa mkao huo mkurugenzi katika shirika la IREMO ambaye pia ni MCA mteule Bi. Darare Gonche amesema kuwa mkutano huo umelenga kuhakikisha kwamba jamii inafahamu kuhusiana na faida za kusajili ardhi ya jamii.

Aidha Darare amekariri kuwa kusajiliwa kwa ardhi pia kutawapa wanawake katika kaunti ya Marsabit haki ya kumiliki ardhi kisheria.

Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la Pastrolist Intergrated Support Program (PISP) Katelo Ibrae Guyo ni kuwa hakuna wadi ambazo zimetengwa katika zoezi hilo linalolenga kuwapa wananchi mammlaka ya kufanya wanavyotaka na ardhi yao.

Hata hivyo Katelo ameweka wazi kuwa hifadhi za jamii haziadhiri kwa vyovyote vile usajili wa ardhi ya jamii.

Mwenyekiti wa Baraza la wazee jamii ya Gabra Shama Boy Wario kwa upande wake amekariri hoja ya jamii kushirikiana katika kufanikisha hili.

Subscribe to eNewsletter