Local Bulletins

VIONGOZI WA KIDINI MARSABIT WAZIDI KUKASHIFU ONGEZEKO LA MAPENZI YA JINSIA MOJA NCHINI.

Na Lelo Wako

Viongozi wa kidini mjini Marsabit wamekashifu kuenea kwa  uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja na visa vya ukahaba haswa miongoni mwa vijana.

Msimamizi wa kanisa la katoliki parokia ya cathedral, Padri Tito Makhoha amekashifu uhusiano aina hiyo huku akiwaomba vijana wasishinikizwe katika kushiriki uhusiano wa jinsia moja.

Ametoa ombi kwa vijana kutoshiriki katika ukahaba na badala ya hiyo kujituma ili waweza kujimudu kimaisha.

Kauli yake padri Tito  imeungwa mkono na imamu wa msikiti wa Jamia, Mohamed Noor.

Amesema kuwa umaskini ni baadhi ya masuala ambayo yanasababisha vijana kujiingiza katika ukahaba.

Sheikh Mohamed amewashauri wazazi kuwalinda vyema wanao na kuwafuatilia wakati huu wa likizo kwa kuwapa wosia na kuwaelekeza vyema.

Pia ametoa wito kwa polisi kuwaadhibu wanaouza dawa za kulevya kwa watoto ili kukuwe na jamii yenye maadili mema.

Subscribe to eNewsletter