Local Bulletins

VIONGOZI WA KIDINI MARSABIT WAUNGA MKONO KUDHIBITIWA KWA DINI NA WAHUBIRI BANDIA.

.Na Samuel Kosgei

Baadhi ya viongozi wa kidini katika kaunti ya Marsabit wameunga mkono mpango wa serikali kudhibiti maeneo ya kuabudu sawa na kuwapiga msasa viongozi wenyewe.

Mwenyekiti wa baraza la makanisa kaunti ya Marsabit Diba Saido akizungumza na idhaa hii amesema kuwa mpango huo wa kudhibiti maeneo ya kidini nchini itasaidia kuwaondoa baadhi ya wahubiri wa urongo na walaghai wanaojificha ndani ya dini za kikristo, kiislamu na hata hekalu za kihindi.

Diba ambaye pia ni mhubiri wa kanisa la Evangelical Lutheran hapa Marsabit anasema kuwa uhuru uliopo unatumiwa vibaya na baadhi ya watu wanaoendesha masuala ya dini nchini hivyo mikakati iliyowekwa na jopo la rais la kutadhmini maeneo ya kuabudia inafaa pakubwa.

Wakti uo huo anasisitiza umuhimu ya wanaotaka kufungua maeneo ya kuabudia kupata elimu ya kidini ili kuendana na maadili ya kijamii na taifa.

Anasema kuwa endapo suala la kudhibitiwa kwa maeneo hayo na hata waliofuzu kupata mafunzo ya theolojia ingekuwepo kutoka mwanzo huenda maafa ya Shakahola hayangetokea.

Kauli yake mhubiri hiyo imesisitizwa na pasta Daudi Wako ambaye ni kasisi katika kanisa la PEFA mjini Marsabit ambaye anasema kuwa ulimwengu wa sasa umejaa manabii wa uwongo na hivyo kuweka mikakati ya kuwaondoa na kuwachuja ni suala la kushabikiwa sana na dini zote.

Ametaka dhehebu hizo zote ziweze kuandikishwa na kusajiliwa upya ili kuwafurusha viongozi walaghai au wale wanaosajili vijana kujiunga na makundi ya itikadi kali kama vile ugaidi.

Subscribe to eNewsletter