Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
ASKOFU wa kanisa la Kianglikana (ACK) kaunti ya Marsabit Wario Daniel Qampicha ameshutumu tabia ya wizi wa mitihani wa kitaifa akisema kuwa tabia hiyo hukuza jamii potovu iwapo haitakomeshwa.
Askofu Qampicha akizungumza na radio jangwani kwenye kipindi cha Amkia Jangwani amesema kuwa kubembeleza tabia ya wizi wa mitihani ya kitaifa ni sawa na bomu inayosubiri kulipuka.
Anasema hilo huchangia kupatikana kwa wataalamu bandia ambao hawajafuzu suala analosema ni hatari mno. Amewataka wanafunzi kukoma kujihusisha na hudanganyifu.
Aidha anasema hulka hiyo huchangia kupatika kwa viongozi wafisadi na wasiowajibika kwani walizoea maisha ya njia mkato yasiyo na uaminifu.
Amewashutumu wazazi ambao hushabikia wizi huo kwani wao ndio hutoa pesa za kununua mitihani.
Kauli yake hiyo imekaririwa na sheikh Mohamed Noor ambaye anasema kuwa ni elimu pekee ndio ina uwezo wa kubadilisha mawazo, mwonekano na hata kuondoa umaskini katika jamii za Marsabit.
atibu wa chama cha kutetea maslahi ya walimu KNUT tawi la Marsabit Rosemary Talaso kwa upande wake ameshutumu wizi wa mitihani huku akikosoa wazazi kwa kukubali kutoa pesa za kuendeleza udanganyifu.
Wakati huo amewataka wazazi kutoshinikiza watoto kupitia mitihani akidai hilo huwapa uoga wanafunzi na kufanya kila wawezalo na kufurahisha wazazi.