Idadi chache ya wanafunzi waripoti shuleni wiki ya kwanza ya muhula huu…
January 10, 2025
BY APIYO EBENET AND JOHN BOSCO NATELENG
Mwanaharakati Nuria Gollo wa MWADO (shirika lisilo la kiserikali) ametoa wito kwa viongozi katika Kaunti ya Marsabit kusitisha malumbano na mvutano wa kisiasa baina yao na kuanza kufanya kazi kwa ushirikiano.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi yake, Nuria amewaomba viongozi kuzika tofauti zao na kushirikiana ili kuzuia mzozo wa kikabila kama ulioonekana mwaka jana.
Aidha, Nuria amewataka viongozi kuacha kampeni za mapema na badala yake kufanya kazi ambayo wamechaguliwa kufanyia wananchi.
Kadhalika, Nuria amewarai wananchi kuwacha kusikiza maneno ya viongozi hawa kwani ndio chanzo cha kuharibu amani inayoonekana katika eneo hilo.
Amesisitiza kuwa ni muhimu vyombo vya habari kuwa makini wakati wa kutoa ujumbe kwa wananchi ili kusaidia kudumisha amani.
Kwa ujumla, Nuria anaona kuwa uafikiano na ushirikiano kati ya viongozi na wananchi ndio njia pekee ya kuleta maendeleo na kuimarisha amani katika Kaunti ya Marsabit.