Mwanaume moja wa miaka 38 ameponea kifo baada ya jaribio la kujitoa uhai kwa kujinyonga kutibuka usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Soweto mjini Laisamis kaunti ya Marsabit.
February 7, 2025
Na Talaso Huka
Vijana wawili wamejeruhiwa usiku wa kuamkia leo baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana. Tukio hilo lilitokea eneo la Karantina, Saku kaunti ya Marsabit.
Akidhibitisha kisa hicho kamanda wa polisi kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo amesema kuwa uchunguzi unaendelea huku akibainisha kuwa lengo la mavamizi hayo hayajulikani.
Hata hivyo amesema kuwa vijana hao wanaendelea kupata matibabu katika hospitali ya rufaa ya Marsabit.