Idadi chache ya wanafunzi waripoti shuleni wiki ya kwanza ya muhula huu…
January 10, 2025
NA GRACE GUMATO
Vijana katika kaunti ya Marsabit wamehimizwa kutoa damu kwa wingi ilikusaidia wale walionao upungufu wa damu.
Akizungumza na idhaa kiongozi wa vijana kutoka kaunti ya Marsabit Abdiaziz Boru amesema kuwa wiki hii ikiwa ni wiki ya kutoa damu ulimwenguni amewahimiza vijana wajitokeze kwa wingi ili kuokoa akina-mama ambao wanajifungua na wale wanahitaji damu na pia kutenga damu nyingi kwa matumizi ya baadaye.
Aidha Abdi amesema kuwa damu ambayo inatolewa wiki hii itasaidia kaunti ndogo ya North Horr, Laisamis na Moyale akisema ni vizuri watu kutoa ili hospitali za rufaa ya Marsabit kuepukana na kununua wa damu kutoka kaunti nyingine.
Hata hivyo vijana kutoka timu ya Chester kaunti ya Marsabit pia wamejitokeza kutoa damu wakisema kuwa kutoa kwa damu itasaidia kuokoa maisha ya watu wanaohitaji damu.
Wiki ya kitaifa ya kutoa damu imeanza siku tarehe 10 Jumatatu wiki hii hadi tarehe 14 mwezi huu ikiwa ni siku ya kutoa damu kote ulimwenguni.
Hafla hiyo hapa Marsabit itaongozwa na waziri wa afya nchini Susan Nakhumicha