Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Na Isaac Waihenya,
Wito wa vijana kutumia vipaji vyao kukabiliana na swala la ukosefu wa ajira umezidi kutotewa huku vijana wakihimizwa kukubatia ajira kidijitali.
Kwa mujibu wa waziri wa elimu katika kaunti ya Marsabit Ambaro Abdulahi ni kuwa kaunti ya Marsabit ina vipaji mbalimbali ambavyo bado havijatambuliwa.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa zoezi la kushereherekea wiki ya vijana, waziri Ambaro ametaja kwamba serekali ya kaunti ya Marsabit imejitolea kuwapiga jeki vijana katika sekta mbalimbali.
Kwa upande wake msimamizi wa maswala ya vijana katika Shirika la CRS Irene Wairimu ni kuwa haflla hiyo ililenga kuwapa vijana fursa ya kujikuza na kupata maarifa ya kutatua swala ya ukosefu wa ajira.
Irene aliwataka vijana kushirikiana na mashirika mbalimbali yasiyoyakiserekali yanayowapiga jeki vijana.