Idadi chache ya wanafunzi waripoti shuleni wiki ya kwanza ya muhula huu…
January 10, 2025
Na Lelo Wako & Elias Jalle,
Vijana katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kutumia wiki ya vijana kuonyesha talanta zao na vipaji walivyo navyo.
Wakiongozwa spika wa bunge la vijana Saku Youth Assembly Abdiaziz Boru, vijana hao wamewataka vijana wenzao kujiunga nao wiki ijayo katika wiki ya vijana ili kuonyesha vipaji na talaza zao kwa wanaMarsabit na hata ulimwengu kwa ujumla.
Abdiaziz Boru ametaja kwamba vijana wengi hapa jimboni wamelalia talanta zao huku akiitaja wiki ya vijana kama itayosaidia katika kuhakikisha kwamba vipaji walivyo navyo vinatambuliwa.
Kwa upande wake Halima Osman anayewakilisha watu wanaoishi na ulemavu amewahimiza vijana wanaoishi na ulemavu hapa jimboni Marsabit kutumia talanta zao kujiendeleza kimapato.