Local Bulletins

USALAMA WAIMARISHWA MPAKANI MWA KENYA NA ETHIOPIA KUFUATIA MAKABILIANO YANAYOENDELEA KATI YA KUNDI LA WAASI LA OROMO, OLF NA WANAJESHI WA ETHIOPIA

NA CAROL WAFORO

Usalama umeimarishwa mpakani pa Kenya na Ethiopia kufuatia makabiliano yanayoendelea kati ya kundi la waasi la Oromo, OLF na wanajeshi wa Ethiopia. Ni makabiliano yanayoendelea katika eneo la Dukale nchini Ethiopia kilomita moja kutoka kaunti ndogo ya Sololo, Kenya.

Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani kaimu kamisha wa jimbo la Marsabit David Saruni amesema kuwa makabiliano hayo wamewaweka wakaazi wa vijiji vya Jillo Wako na Wario Guyo katika hofu kubwa.

Kundi la waasi la Oromo, OLF kutoka nchi ya Ethiopia huwa na hulka ya kukimbilia Kenya kufuatia makabiliano baina yao na wanajeshi wa Ethiopia na kusababisha hofu ya utovu wa usalama.

Saruni anasema kuwa kwa hivi sasa hakuna taarifa ya waasi hao wa OLF kuvuka mpaka kuingia humu nchini Kenya.

Aidha Saruni amedokeza kuwa wanajeshi wa Kenya KDF kwa ushirikiano na maafisa wa usalama wanashika doria ili kuwakakikishia wakaazi wa vijiji hivyo usalama wao.

Itakumbukwa kuwa majuma kadhaa yaliyopita watoto watatu walipata majeraha kule Anona eneo la Sololo kaunti ya Marsabit baada ya kundi hilo kukimbilia Kenya kufuatia makabiliano baina yao na wanajeshi wa Ethiopia na kusababisha utovu wa usalama.

Subscribe to eNewsletter