Marsabit yatajwa kuwa miongoni mwa kaunti zinazokuwa kwa kasi kimaendeleo.
January 15, 2025
Ulimwengu waadhimisha siku ya walemavu jana,huku wito wa kuwapeleka watoto walemavu shuleni ukisheheni…
Wakaazi katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kuwapeleka wanao shuleni punde tu shule zitakapofunguliwa kwa muhula wa kwanza mwaka ujao wa 2025
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa elimu katika kaunti ndogo ya Bubisa katika kaunti ya Marsabit Jillo Abdi ni kwamba bado kunao watoto ambao wamefungiwa manyumbani na kunyimwa haki yao ya elimu.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuadhimisha siku ya walemavu duniani katika kaunti ya Marsabit iliyoandaliwa katika ukumbi wa kanisa Katoliki hapa mjini Marsabit,Jillo ametaja kwamba ni haki ya kila mtoto kupewa elimu ili waweze kujifaidi katika maisha yao ya baadae.
Kauli yake Jillo imeshambikiwa na afisa msimamizi wa baraza la watu wanoishi na ulemavu National Council for Persons with Disabilities (NCPLD) kaunti ya Marsabit Abdi Ahmed ambaye ameonya dhidi ya kuwanyiwa watoto wanaoishi na ulemavu haki yao ya elimu.