Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Mkumbo wa kwanza wa madarasa ya gredi ya 9 katika kaunti ya Marsabit umekamilika kwa asilimia 100 huku mkumbo wa pili ukiwa umekamilika kwa asilimia 56.
Haya ni kwa mujibu wa mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit Peter Magiri ambaye amewataka wazazi kutokuwa na hofu kuhusiana na swala la madarasa ya gredi ya tisa kabla ya shule kufunguliwa kwa muhula wa kwanza wa 2025.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya simu, Magiri ametaja kwamba mkumbo wa pili umechelewa kukamilika kutokana na serekali kuchelewasha mgao wa fedha wa kuendeleza zoezi hilo huku akiahidi kuwa wa ujenzi wa madarasa hayo utakamilika wiki ijayo.
Aidha Magiri ameweka wazi kuwa mkumbo huu wa pili unalenga kuongeza madarasa 70 zaidi huku maradasa 36 ya mkumbo wa kwanza yakiwa yako tayari kwa matumizi.