Local Bulletins

THE TIIGO SCHOOL NDIO MABINGWA WA MARSABIT SCIENCE FAIR 2024…

Na Isaac Waihenya,

Msimamizi wa kiwango cha ubora wa elimu katika kaunti ya Marsabit Mumas Wanyama ameuchangamoto usimamizi wa hazina ya maeneo bunge CDF katika kaunti ya Marsabit kuhakikisha kwamba kila shule ya msingi nganzi ya juu JSS ina maabara.

Akizungumza katika shule The Tiigo eneo la Turbi wakati wa hafla ya mashindano ya shule za JSS ya uvumbuzi wa kisayansi (Science Fair) kuhusiana na jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi iliyofadhiliwa na Shirika la Concern World Wide,Wanyama ametaja kwamba uwepo wa maabara utapiga jeki masomo ya sayansi.

Wanyama hata hivyo amesifia ustadi na hatua zilizopigwa na shule zilizoshirika mashindano ya mwaka huu.

Kauli yake Wanyama imeshabikiwa na meneja wa masomo katika Shirika la Concern Worldwide Catherine Akasa ambaye ametaja kwamba shirika hilo litaongezea idadi ya wanaoshiriki katika shindano hilo ili kuhakikisha kwamba wanapiga jeki masomo ya sayansi katika maeneo kame.

Adha mwakilishi wa mbunge wa North Horr aliyehudhuria hafla hiyo ameweka wazi kwamba watashirikiana na mashirika yasiyo ya kiserekali jimboni ili kuhakikisha kwamba kiwango cha elimu katika eneo bunge hilo kinaimarika.

Katika mashindano ya mwaka huu shule ya The Tiigo iliibuka na ushindi katika mradi wao uvumbuzi unaolenga kubuni mbinu mbadala za upishi kuliko kutumia kuni ili kuhifadhi mazingira.

Joseph Kinyua ni mwalimu wa wanafunzi wawili waliopata ushindi.

Hata hivyo wanafunzi wawili walioibuka washindi makala ya 2024 Fatuma Leleka na Mola Boru hawakuficha furaha yao.

Subscribe to eNewsletter