Local Bulletins

Tamaduni na mila za jamii za Marsabit sasa kuhifadhiwa kidijitali kwa ajili ya kizazi kijacho.

.

Na Samuel Kosgei

 

Serikali ya kaunti ya Marsabit ikishirikiana na Taasisi ya makavazi za kitaifa National Museum Of Kenya (NMK) imeweka makubaliano ya kushirikiana kuweka utamaduni na mila za jamii 10 asilia za Marsabit katika hifadhi ya kidigitali kinyume ilivyo Kwa Sasa ambapo tamaduni hizo hazijahifadhiwa kidigitali.

Waziri wa Utalii na utamaduni kaunti ya Marsabit Jeremiah Ledaanyi amesema ni hatua ya kufurahia kuona serikali ya kaunti na serikali kuu ikitambua Mila Na tamaduni ya jamii za Marsabit.

Makundi ya vijana kutoka jamii za Marsabit yamepitia mafunzo ya kunakili, kuweka na kuhifadhi siri za jamii hizo 10 bila kutumia kujifaidi.

Jamii hizo 10 ambazo utamaduni wao utahifadhiwa kidigitali ni pamoja na: Borana, Rendile, Gabra, Burji, Sakuye, Konso Daasanach, Elmolo, Sitama na Wayyu.

Waziri Ledanyi amesema Jamii nyingine 4 ambazo zimesalia kama vile Samburu, Turkana, Somali na Garre tayari historia yake na tamaduni zao zimehifadhiwa katika kaunti nyingine.

“Jamii ya Samburu, Turkana, Somali, Garre tumetoa kwa sababu utamaduni wao umehifadhiwa tayari katika kaunti za Samburu, Turkana, Garissa, Wajir na Mandera mtawalia” akasema waziri Ledanyi.

Mkurugenzi Wa Taasi ya makavazi ya kitaifa Edwin Obonyo, Naibu gavana wa Marsabit Solomon Gubo, Waziri wa Utalii na utamaduni Jeremiah Ledaanyi wameshuhudia kutiwa sahihi Kwa makubaliano hayo.

Subscribe to eNewsletter