Local Bulletins

Takriban vijana 1,500 jimboni Marsabit wanatarajiwa kunufaika na kazi mazingira

Takriban vijana 1,500 jimboni Marsabit wanatarajiwa kunufaika na kazi mazingira mpango wa kushughulikia hali ya anga na ambao ulizinduliwa na rais William Ruto mwezi septemba.

Mpango huu ni mojawepo ya mbinu ya kuunda nafasi za kazi kwa mamilioni ya vijana ambao hawajaajiriwa nchini na ambao ulichukua nafasi ya Kazi Mtaani mpango wa rais mstaafu Uhuru Kenyatta.

Haya yamewekwa wazi na mhifadhi wa msitu kaunti ya Marsabit Mark Lenguro ambaye amesema kuwa mpango huu unatarajiwa kungoa nanga humu jimboni Marsabit hivi karibuni.

Kulingana naye vijana hawa watahusika katika utunzaji wa mazingira huku wakitarajiwa kulipwa shilingi 600 kwa siku.

Subscribe to eNewsletter