Mwanaume moja wa miaka 38 ameponea kifo baada ya jaribio la kujitoa uhai kwa kujinyonga kutibuka usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Soweto mjini Laisamis kaunti ya Marsabit.
February 7, 2025
Na Isaac Waihenya,
Wananchi katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kutunza amani ambayo imekuwa ikishuhudiwa kwa muda hapa jimboni.
Kwa mujibu wa ACC wa eneo la Gadamoji Thomas Ngang’i ni kuwa ni jukumu la kila mwanchi kuhakikisha kwamba amani imesheheni hapa jimboni Marsabit.
Akizungumza wakati wa mkao uliwaleta pamoja washikadau kutoka sekta mbalimbali jimboni, Ngang’i ametaja kwamba visa vya utovu wa usalama ambavyo vimeshuhudiwa hapa jimboni hivi maajuzi ikiwemo kile cha eneo la Elle-Dimtu ambapo watu 8 waliuwawa na kisha kuteketezwa pamoja na jaribio la wizi wa pikipiki karibu na shule ya SKM hapa jimboni Marsabit ni tishio kwa usalama wa jimbo hili, huku akiwataka wananchi kutoa ripoti kwa maafisa wa usalama ili kuhakikisha kwamba usalama unadumishwa.
Ngang’i amewataka wananchi pia kushirikiana kwa karibu na asasi za kiusalama kwa lengo la kuboresha amani na uiano katika kaunti ya Marsabit.