Local Bulletins

SHULE YA MSINGI YA MARSABIT INAHITAJI UKARABATI NA VYOMBO VYA KUTOSHA

NA CAROLINE WAFORO

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Marsabit, Bw. Abdi Ano, ametoa wito wa kukarabatiwa na kuboreshwa kwa shule hiyo.

Akizungumza katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani iliyofanyika shuleni, Bw. Ano amelalamikia ukosefu wa miundombinu muhimu kama vile madarasa na vyoo.

Amebainisha kuwa takribani wasichana 256 wanautumia vyoo viwili pekee, jambo linaloweka afya yao hatarini. Aidha, amesema kuwa kuna upungufu wa walimu, hali inayoathiri ufundishaji kwa wanafunzi.

Vilevile, Mwalimu Ano amebainisha kuwa shule hiyo ina mabonde mengi ambayo huwafanya wanafunzi kuwa katika hatari wakati wa msimu wa mvua.

Kwa hivyo, Mwalimu Mkuu amewataka wanaohusika kuchukua hatua haraka ili kukarabati na kuboresha miundombinu ya shule ya Msingi ya Marsabit ili kukabiliana na changamoto hizo na kuboresha ubora wa elimu kwa wanafunzi.

Share

Subscribe to eNewsletter