Mwanaume moja wa miaka 38 ameponea kifo baada ya jaribio la kujitoa uhai kwa kujinyonga kutibuka usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Soweto mjini Laisamis kaunti ya Marsabit.
February 7, 2025
Na Isaac Waihenya & Ali Ibrahim
Shughuli za kawaida zimerejea katika hospitali ya rufaa ya Marsabit baada ya maafisa wa kliniki kurejea kazini.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na Radio Jangwani wameeleza kwamba kwa sasa hali imeimarika na wamapata huduma za afya kama inavyaostahili.
Wametaja kurejea kwa maafisa hao kama afueni kwao kwani hawalaziki kutembelea hospitali za kibinafsi kusaka matibabu.
Maafisa wa kliniki wamerejea kazini hii Leo baada ya kuwa kwenye mgomo kwa kipindi cha miezi minne, hii ni baada ya maelewano kati ya maafisa hao na idara ya Afya yaliyotiwa saini siku ya jumatatu.