HEMORRHAGE (PPH) NDIO CHANZO KIKUU CHA VIFO MIONGONI MWA KINA MAMA WANAPOJIFUNGUA.
October 11, 2024
Na Carol Waforo
Katika juhudi za kuwahakikishia wakaazi wa Kaunti ya Marsabit usalama wao wa chakula serikali inapanga kufanya miradi mbalimbali ya maji itakayopiga jeki ukulima.
Hii ni pamoja na kujenga mabwa pamoja na kuchimba visima vya maji katika maeneo tofauti humu Jimboni Marsabit.
Haya yamebainika katika uzinduzi wa nne wa mpango wastani ambao unajumuisha kipindi cha mwaka 2023-2027, kikao cha kuhusisha umma na ufafanuzi wa programu ya maendeleo katika kaunti ya Marsabit, hafla iliyoandaliwa katika ukumbi wa kanisa katoliki.
Huu ni mpango wa nne wa sehemu kadhaa za kenya kwenye ruwaza ya mwaka 2030.
Akieleza mipango ya serikali katika mpango huo katibu wa maeneo kame na ustawi wa kimaeneo Kello Harsama amesema kwua ruwaza hiyo itaendana na mfumo wa seriklai wa kuimarisha uchumi wa bottom up.
Kello pia amesema kuwa serikali imetenga Shilingi millioni 300 zitakazo fanikisha ujenzi wa mahala pa kuendeleza biashara ya samaki.
Kadhalika Kello amesema idara yake kwa ushirikiano na serikali ya Uholanzi na serikali kuu pia imetenga shilingi 1.5 kupiga jeki shughuli za uvuvi.
Waziri wa usalama wa kitaifa Kithure Kindiki, katibu wa maeneo kame Kello Harsama, gavana Mohamud Ali, naibu gavana Solomon Gubo, kaimu kamishna wa Marsabit David Saruni walihudhuria.
Aidha mawaziri mbalimbali katika serikali ya gavana mohamud Ali pia walihudhuria kati ya Viongozi wengine.