SERIKALI YASISITIZA KUWA CHANJO YA MIFUGO INALENGA KUPANUA SOKO LA MIFUGO LA KIMATAIFA.
December 18, 2024
Serikali imesisitiza haja ya mifugo yote nchini iweze kupewa chanjo ili kupanua soko la mifugo la kimataifa.
Rais William Ruto akizungumza hii leo katika soko kuu la mifugo ya Kimalel kaunti ya Baringo amesema kuwa chanjo inayoenda kufanyika January mwaka ujao inalenga kuzuia ugonjwa wa mifugo huku akipuuzilia mbali wanaokosoa programu hiyo akiwataja kama maadui wa maendeleo na wasiotakia wakenya makuu.
Akitetea zoezi hilo, katibu katika idara ya mifugo Jonathan Mweke amesema kuwa kuna soka kubwa la mifugo katika mataifa uarabuni ila hitaji ni kuwa lazima mifugo ipewe chanjo ili isisambaze magonjwa ambukizi kama foot n mouth.
Katibu mweke amekariri kuwa chanjo hiyo ya mifugo inatengenezewa hapa nchini hivyo hamna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu athari ya chanjo hizo. Ameomba wakosoaji kuacha uvumi na propaganda kuhusu chanjo hiyo.