Local Bulletins

SERIKALI YA MARSABIT YAPANGA MASHINDANO YA KIDIGITALI MAARUFU HACKATHON NA KUELIMISHA VIJANA KUHUSU MASWALA YA KIDIGITALI

Na huku vijana wakiendelea kujipanga kwa ajili maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana serikali ya kaunti ya Marsabit kupitia idara ya michezo na maswala ya vijana imesema kuwa imepanga hafla mbalimbali kwa ajili ya siku hiyo.

Akizungumza na shajara ya radio Jangwani afisini mwake kaimu mkurugenzi wa idara hiyo Daud Iman amesema kuwa wanapanga mashindano ya kidigitali maarufu hackathon pamoja na kuelimisha vijana kuhusu maswala ya kidigitali kuendana na kauli mbiu ya mwaka huu “Vijana na Matumizi ya fursa za Kidigitali kwa Maendeleo endelevu,”

Aidha anasema kuwa vijana watapata fursa ya kuuza talanza zao kwa washikadau mbalimbali watakaohudhuria mashindano hayo huku pia akiwachangamoto vijana kutumia teknolojia zilizopo kujiajiri.

Kadhalika amewataka vijana katika kaunti hii ya Marsabit kujiepusha na utumizi wa dawa za kulevya huku akitoa hamasa kwa vijana kuhakikisha kuwa wanahudhuria hafla za ushirikishwaji wa umma ili kuhakikisha kuwa wanatoa mapendekezo ya miradi mbalimbali inayowahusu.

Vijana wametakiwa kutumia wiki hiyo ya tarehe 12 Agosti kuonyesha talanta zao na vipaji walivyo navyo.

Subscribe to eNewsletter