Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Kuna haja ya kuelimisha wakazi wanaoishi karibu na Jangwa la Chalbi, jimboni Marsabit kuhusu umuhimu wa kupanda miti. Haya ni kwa mujibu wa naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Maikona Pius Njeru
Njeru amesema kuwa bado wakazi wanaoishi katika maeneo ya Chalbi hawajakumbatia mpango wa upanzi wa miti jambo ambalo ameelezea kuwa ni changamoto kwa serekali na mashirika yasiyo ya kiserekali ambayo yanaleta msaada wa upanzi wa miti katika maeneo hayo.
Akizungumza na idhaa hii, Njeru ameitaka baraza la wazee wa maeneo hayo kushirikiana pamoja na serekali ili kutoa hamasa kwa wakazi hawa kuhusu umuhimu wa kupanda miti.
Njeru amesema kuwa uhaba wa maji katika eneo la Chalbi ndio pia chanzo cha wakazi kukosa kukumbatia upanzi wa miti, hivyo kutoa wito kwa washikadau tofauti kuipa swala la Maji katika eneo hilo kipaumbele.
huku msimu wa sherehe ya krismasi na mwaka mpya ukiwadia Njeru amesema kuwa usalama unazidi kuboreshwa katika eneo la Marsabit North na kuwataka wakazi kuripoti visa vyovyote vya uhalifu kwa idara ya usalama iliyo karibu nao.