Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Serikali kuu inafanya kila jitihadi kuhakikisha kuwa wakimbizi wa ndani kwa ndani kaunti ya Marsabit wanapata msaada wa chakula na mahitaji ya msingi.
Akizungumza katika hafla ya kuwapokeza familia 50 mabati 30 na kanisa la kianglikana, Naibu Kamishena wa Marsabit Central David Saruni amesema kuwa wakimbizi hapa Marsabit wanapitia changamoto nyingi huku akisema kuwa serikali bado inawakumbuka wakimbizi hao kwa chakula cha msaada na misaada mingine.
Aidha Saruni amesema kuwa wale ambao wameadhirika na vita vya kikabila ni akina mama na watoto huku akiomba jamii za Marsabit kukumbatia Amani kila wakati ili idadi ya wale wanaoadhirika na vita vya kikabila visiongezeke.
Hata hivyo Saruni amewahakikishia wakimbizi hao kuwa mashamba yao bado yapo na hakuna mtu yeyote atakaye wanyanganya na pia kuwaomba wahisani kuwapiga jeki wakimbizi hao kwa misaada Zaidi.