Local Bulletins

SEREKALI YA KAUNTI YA MARSABIT IMETAKIWA KUHAKIKISHA KUWA WATU WANAOISHI NA ULEMAVU WAMEWAKILISHWA KIUKAMILIFU.

Na JB Nateleng,

Serekali ya kaunti ya Marsabit ni sharti ihakikishe ya kwamba watu wanaoishi na ulemavu wamewakilishwa katika idara zote kiukamilifu.

Hayao yamekaririwa na mwenyekiti wa muungano wawatu wanaishi na ulemavu wa Saku United Disabled Group John Boru Galgallo.

Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipee Boru amesema kuwa bado watu wanaoishi na ulemavu hawajawakilishwa vyema jimboni Marsabit jambo ambalo linalemaza utoaji wa huduma kwa watu wanaoishi na ulemavu.

Boru ameelezea kuwa pia bado watu wanaoishi na ulemavu hawapati huduma muhimu kutoka kwa serekali ya kaunti ya Marsabit kwa sababu ya kutokuwepo na mtu ambaye anawakilisha na kufikisha malalamishi yao katika ofisi husika.

Hata hivyo Boru ametoa wito kwa serekali ya kaunti ya Marsabit na mashirika yasiyo ya kiserekali kuhakikisha kuwa haki za watu wanaoishi na ulemavu zimetiliwa maanani na kutimizwa kama za wananchi wengine.

Subscribe to eNewsletter