Serikali ya kaunti ya Marsabit yakana madai ya unyakuzi wa ardhi na kutenga jamii ya Sakuye katika harakati ya kufunguliwa kwa mgodi wa Dabel.
January 13, 2025
Na Samuel Kosgei
SENETA wa Marsabit Mohamed Chute amesema yuko tayari kujiuzulu iwapo tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC itaweza kudhibitisha kuwa alipokea malipo ya shilingi milioni 365 kama ilivyodaiwa wiki jana.
Seneta Chute akizungumza na idhaa hii kwenye kipindi cha Amkia Jangwani asubuhi ya Jumatano amesema kuwa yeye hakukamatwa na maafisa wa EACC bali alijiwasilisha mbele ya tume hiyo kujibu tuhuma zinazomhusu gavana wa Marsabit Mohamud Ali.
Ameshutumu tume hiyo ya EACC kwa utepetevu huku akidai inatumika kusema urongo na kueneza propaganda dhidi ya ofisi yake.
Wakati uo huo amezidi kushutumu serikali ya kaunti kwa kutolipa makato ya pesa ya wafanyakazi wa kaunti licha ya kukata mchango wao wa NHIF, NSSF na hata mikopo yao ya benki.
Ameambia shajara kuwa pesa hizo za makato ni takribani shilingi milioni 34 na hafahamu ni kwani nini hela hizo halipiwi licha wa wafanyakazi kukatwa.
Analaumu utepetevu na madai ya ufisadi
Kuhusiana na mrundiko wa madeni yanayodaiwa serikali na wafanyakazi ikiwemo wahudumu wa afya, wanagenzi na wengineo seneta Chute amekana kuwa sababu sio kuchelewa kwa mgao wa serikali kuu kama utawala wa gavana Ali ulivyojitetea siku za nyuma. Anasema mgao karibu wote wa kaunti ushatumwa kwa akaunti za kaunti.