Wakazi wa vijiji vya Nawapa,Kulamawe na Kilimambogo Loiyangalani,wamelalamikia uhaba wa maji…
January 15, 2025
Saratani ya Umio ndio Saratani inayoongoza katika Kaunti ya Marsabit kwa Asilimia 33 ikifutwa na saratani zinazoanzia sehemu ya shingo kwenda sehemu ya kichwa kwa asilimia 19.
Akizungumza na idhaa hii Joyce Makoro ambaye ni afisa anayesimamia kliniki ya saratani katika hospitali ya rufaa ya Marsabit ni kuwa idadi ya wanawake walioadhirika na saratani hii ni asilimia 43 huku wanaume walioadhirika ni asilimia 23 kulingana na data mwaka 2021.
Aidha Makoro amesema kuwa saratani ya umio unasababishwa na mambo kadha kama vile umri, pombe, uvutaji wa sigara, Kunenepa kupita kiasi na pia kukula chakula zilizopakiwa.
Hata hivyo Makoro amesema dalili za saratini ya umio ni Maumivu kwenye koo au mgongo, kuumwa na kifua au katikati ya mbega kutapika au kukohoa damu, kukua kikohozi cha muda mrefu na pia Kupunguza uzito bila kusudia.