Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Na Samuel Kosgei
Vijana wanagenzi walioajiriwa na serikali ya kaunti kwa kandarasi ya mwaka mmoja wameendelea kutoa lalama zao ya kutolipwa marupurupu ya zaidi ya miezi sita.
Wanagenzi hao ambao leo wamefanya kikao na kamati ya bunge la Marsabit kuhusu utawala wamerai wawakilishi wadi wao kuwasaidia kusukuma serikali kuwapa malipo yao ambayo kufikia sasa wamelipwa miezi mine pekee.
Baadhi yao wamedai kuwa wamelipwa miezi miwili pekee huku wenzao wakilipwa miezi minne.
Walitaka kujua mpango uliopo ili kulipwa marupurupu kabla ya kandarasai yao kukamilika mwezi September.
Nasibo Dokata Ramata mmoja wa vijana hao ameeleza masaibu yao ambayo ni pamoja na kucheleweshwa kwa marupurupu yao, kukatwa kwa pesa zao za NHIF na NSSF lakini makato hayo hayafiki kwenye hazina husika.
“Tumefika bungeni kujua mbona pesa zetu zimechelewa ilhali kandarasi yetu inakamiliki mwezi ujao. Tunadai kama miezi minane sasa” Alisema Nasibo.
Anasema kuwa wana Imani MCAs wao watawasaidia kupata haki hiyo ambayo kwa muda wamekuwa wakisaka.Mwenyekiti wa kamati ya Utawala Joseph Leruk ameondolea lawama bunge kwani wao walitenga pesa hizo kwenye bajeti ya mwaka jana ila serikali ya jimbo ndio iliyoweka pesa zao kusikofaa.
Leruk amesema kuwa mwishoni mwa wiki ijayo pesa za miezi miwili italipwa huku lengo kuu likiwa kuhakikisha vijana hao wanapata malipo yao yote kabla ya muda wao wa kuhudumu kukamilika.
Kamati hiyo pia imeahidi kusaidia vijana Hao kufanya kikao na gavana Wa Marsabit Mohamud Ali na idara nzima ya fedha ili kusaka suluhu Kwa vijana Hao watakaokamilisha kandarasi Yao mwezi ujao.Jacob Elisha ambaye ni MCA wa Marsabit Central amejukumishwa na kamati hiyo kuwaunganisha vijana na gavana wa marsabit pamoja na idara nzima ya fedha.
Mwanzoni tulikuwa na tatizo na mdhibiti wa bajeti baada ya kaunti kuweka pesa za vijana kwenye kikapu cha maendeleo badala ya kapu la matumizi ya kila mwaka” akasema Elisha Godana.
Mwanachama mwingine wa kamati hiyo ambaye ni MCA wa North Horr Tura Ruru amesema watahakikisha kuwa vijana wanapata haki yao japo amewarai vijana kutotumia lugha ya matusi kushambulia viongozi bila kujaribu mbinu ya mazungumzo mwanzo.
Sasa vijana hao wanagenzi kwa sasa wanasubiri kuona kama watapata mwaliko kutoka kwa gavana ili wawe na mkao mmoja wa kufahamu hatma ya malipo yao.