Local Bulletins

NEMA YATIA MBARONI WATU 12 KATIKA KAUNTI YA MARSABIT WAKIWA NA KARATASI ZA PLASTIKI ZILIZOPIGWA MARUFUKU

NA ISAAC WAIHENYA

Watu 12 wamekamatwa na karatasi za plastiki hapa mjini Marsabit kwenye msako uliofanywa na mamlaka ya kutunza mazingira nchini NEMA mchana wa leo.

Kumi na wawili hao wametiwa mbaroni baada ya NEMA kuaandaa zoezi la ukaguzi kuhusiana na uchafuzi wa mazingira katika taasisi mbalimbali pamoja na eneo la kibiashara hapa mjini Marsabit lililongozwa na mkurugenzi mkuu wa NEMA kutoka makao makuu jijini Nairobi Daktari Ayub Macharia.

Akizungumza na meza ya Radio Jangwani Daktari Macharia ametaja kwamba wamelazimika kuandaa zoezi hilo kutoka na idadi kubwa ya wanaopuuza maagizo ya NEMA.

Daktari Macharia ameahidi kuwa mamlaka hiyo imejitolea kuhakikisha kwamba hakuna uchafuzi wa mazingira na wanaokosa kufuata kanuni hitajika wanachukuliwa hatua kali za kisheria japo amekiri kuwepo kwa changamoto katika kaunti zilizopo mipakani.

Kadhalika mkuu huyo wa NEMA ametaja kwamba mamlaka hiyo inashirikiana na idara ya usalama ili kuzidisha msako katika barabara kuu ya Moyale – Isiolo.

Subscribe to eNewsletter