Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Ndotto Warriors ndio mabingwa wa taji la Ahmed Kura Tournament mwaka 2024 baada ya kuilaza timu ya Mt Kulal kwa goli moja kwa nunge kupitia tuta la penalti katika mechi iliyogaragaziwa kwenye uga wa michezo wa Ngurunit,eneo bunge la Laisamis kaunti ya Marsabit.
Mechi hiyo ilikamilka sare tasa ya 0-0 katika muda wa kawaida dakika tisini huku walinda lango watimu zote mbili wakiokoa mashuti kadhaa yaliyoelekezwa kwao wakati wa matuta ya penalti.
Ntotto FC imetia kibindoni shilingi elfu 50 huku Mt Kulal wakitia kibindo shilingi elfu 25 kabla ya nyongeza.
Kwa upande wa akinadada timu ya Loi Queens kutoka eneo la Loiyangalani ilinyakuwa taji hilo baada ya kuilaza Ndotto Queens ya Ngurunit kwa jumla ya magoli 3-0 kwenye fainali.
Upande wa voliboli timu ya voliboli ya Loiyangalani upande wa wanaume ilitwa ubingwa baada ya kuilaza Mt Kulal kwa seti tatu kwa nunge huku akinadada wa Loi Queen wakitamba na kuilaza timu ya voliboli ya Ndotto Queens kwa seti mbili kwa moja.
Katika mchezo wa Darts timu ya Loiyangalani iliishinda timu ya Southhorr huku mshindi alienda nyumbani na shilingi elfu 5.
Katika mpira wa kikapu kikosi cha Korr kilitwa ubingwa baada ya kuilaza timu ya kutoka South-Horr kwa pointi 56 kwa 10.
Akizungumza wakati wa kuwatuza washindi mbalimbali katika Makala hayo ya mwaka wa 2024, mkurugenzi wa shirikia lisilo la kiserekali la Kenya Dryland Education Fund (KDEF) Ahmed Kura amepogeza wote walioshiriki michuano hiyo kwa kuonyesha umoja na uzalendo.
Kura ametaja kwamba lengo la michuano hiyo ni kuhumiza umoja na uiano kati ya jamii mbalimbali zinazoishi ha pa jimboni Marsabit.
Hata hivyo Ahmed Kura ametaja kwamba wanalenga kubuni kikosi kitakachowakilisha eneo hilo hata kwenye michuano ya kitaifa.
Aidha baadhi ya wachezaji wakiongozwa na Lucia Jumapili wa timu ya Loi Queen kutoka Loiyangani wamepongeza hatua ya kuwaleta vijana pamoja wakitaja kuwa hilo linajenga uoiano baina yao.