SERIKALI YASISITIZA KUWA CHANJO YA MIFUGO INALENGA KUPANUA SOKO LA MIFUGO LA KIMATAIFA.
December 18, 2024
Naibu gavana wa Isiolo James Lowassa aelezea hofu kuhusu chanjo ya mifugo inayolenga mifugo mwakani.
Huku mjadala kuhusu utata wa chanjo kwa mifugo ukiendelea humu nchini, naibu gavana wa kaunti ya Isiolo James Lowassa ameelezea wasiwasi wake kuhusu chanjo hiyo akidai kuwa jamii ya wafugaji haijahamasishwa vyema wala kuhusishwa.
Lowassa ametoa changamoto kwa serikali kufanyia chanjo hiyo uchunguzi wa kutosha isije ikawa na madhara yoyote kwa mifugo huku pia akitaka wananchi wahusishwe kikamilifu kwa kuwa ndio wenye mifugo
Wakati uo huo Lowassa amewahimiza wabunge kutopitisha sheria ambayo itawaumiza wakaazi katika kaunti za wafugaji.
Serikali imepanga utoaji wa chanjo kwa mifugo nchini litakaloanza Januari mwaka ujao, 2025
Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, Andrew Karanja ametetea vikali zoezi hilo akisema dawa itakayotumika inaundiwa Kenya.
Kinyume na uvumi kwamba shughuli hiyo ina ajenda fiche, Waziri Karanja amesema inalenga kuboresha usalama wa bidhaa za mifugo nchin