Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Mwandishi wa habari wa Radio Jangwani Isaac Waihenya ashinda tuzo katika tuzo za AGJK….
Mwandishi wa habari wa Radio Jangwani Isaac Waihenya, ameshinda tuzo ya Makala bora chini ya kitengo cha afya katika tuzo zilizotolewa na shirika la Association of grassroot journalist of Kenya AGJK iliyofanyika katika kaunti ya Mombasa wikendi.
Waihenya ameelezea kuwa tuzo hilo lina umuhimu zaidi kwake, Redio Jangwani na pia wasikilizaji ambao wamekuwepo kila mara katika hatua za kuboresha maisha ya WanaMarsabit.
Waihenya amewataka wanahabari wote katika jimbo la Marsabit kuweza kutia bidii na kujituma katika kufanya makala ambayo yanatoa funzo na pia kubadili maisha ya wanajamii n ahata kuangazia yanavyotendeka katika jamii bila kuegemea upande wowote.
Hata hivo Waihenya amepongeza uongozi wa kituo cha habari cha Radio Jangwani pamoja na wanahabari wenzake ambao wamemsaidia katika kuikuza na kuiboresha taluma yake katika tasnia ya uanahabari.