Idadi chache ya wanafunzi waripoti shuleni wiki ya kwanza ya muhula huu…
January 10, 2025
NA GRACE GUMATO
Mwanaume mwenye umri wa makamu amefikishwa katika Mahakama Ya Marsabit hii leo kwa kosa la wizi.
Mshukiwa Diba Guyo anadaiwa kuwa mnamo tarehe 18 mwezi machi mwaka 2024 katika eneo la Manyatta Jillo kaunti ya Marsabit na wengine ambao hawakuwa mbele ya mahakama waliweza kuiba vifaa vya gari inayogharimu shillingi 45,000 mali ya mlalamishi Aden Chukulisa.
Mshukiwa alifikishwa mbele ya hakimu mkuu Christine Wekesa na kukana mashataka dhidi yake huku mahakama ikimwachilia kwa dhamana ya shillingi 50,000 ama pesa taslimu ya shilling 30,000.
Wakati uo huo Did Ali Diba amefikishwa katika mahakama ya Marsabit kwa kosa la kutishia kuua ambalo ni kinyume na sheria.
Mshukiwa anadaiwa kuwa mnamo tarehe 18 mwezi wa Mei maeneo ya Sagante kaunti ya Marsabit alitumia maneno ya kutishia kuua mlalamishi George Guyo.
Mshukiwa alifikishwa mbele ya hakimu mkuu Christine Wekesa na kukana mashataka dhidi yake huku mahakama ikimwachilia kwa pesa taslimu ya shillingi 30,000 kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa tarehe 1 mwezi ujao.